• Mada hii inazungumzia: Haki za binadamu katika uislam amezungumzia maana ya haki na umuhimu wa kujuwa haki za binadamu na ulazima wa kuzilinda, pia ametaja haki tano katika Quraan kwa ujumla.
• Mda hii inazungumzia: maana ya binadamu na maana ya uislam, na ametaja mafundisho ya uislam kuhusu haki za binadamu.
• Amezungumza kuwa uislam ndio wakwanza kufundisha haki za binadam, Haki ya kwanza (Haki ya kuishi).
• Mada hii inazungumzia: Uharam wa kujiua na niharam kutumia kitu ambacho kitamsababishia kifo, kama kuvuta sigara na pombe nk, pia amezungumzia haki ya pili (Kulinda mali za watu) na uharam wa kudhulumiana.
• Mada hii inazungumzia: Uharam wa kudhulumiana na chanzo chake, pia amezungumzia uharam wa kula riba na njama za nchi zilizo endelea katika kula riba, pia kazungumzia uharam wa kula rushwa, na dhulma nimaradhi yanayo ambukiza.
• Mada hii inazungumzia: Haki za binadamu ikiwemo mwanamke kuheshimiwa utu wake, amebainisha hali ya mwanamke kabla ya uislam, na jinsi uislam ulivyo linda heshima ya mwanamke, kabainisha jinsi mwanamke anavyo dhalilisha mwanamke katika karne ya 21.
• Mada hii inazungumzia: Haki za binadamu ikiwemo haki ya kuabudu, na amebainisha kuwa hakuna kulazimishana, kasha akataja hali ya ulinganiaji wakati wa mtume na uongo wa wale wanao sema uislam ulienezwa kwa upanga, bali uislam uliingia kwa hoja zenye nguvu.
• Mada hii inazungumzia: Haki za binadamu nayo nihaki ya mwanadamu kuwa huru, na msingi wa uhuru wa binadamu, ambayo inatolewa katika maneno ya Omar bin Khatwabi (r.a).