1- Mada hii inazungumzia: Neema za nyumba na faidazake, nakwamba nyumba niukamilifu wa neema za Allah kwa waja wake, pia imezungumzia baadhi ya faida za nyumba kama vile makazi, stara, kulala, ibada ya swala na ibada ya ndoa.
2- Mada hii inazungumzia: Nyumba ni sehem ya kumstiri mwanamke na kumlinda na swala iliyo bora kwa mwanamke ni nyumbani, na wanawake wema ni wale wenye kutulia majumbani mwao, pia imezungumzia umuhimu wa kuwafundisha dini na adabu wake na watoto katika majumba.
3- Mada hii inazungumzia: Umuhimu wa kuwafundisha wanawake na watoto mambo ya Sunna na mavazi ya stara ili kuepuka masuuliya siku ya Qiyama, pia imezungumzia ubora wa kulazimiana na nyumba na kutenga muda kwa ajili ya kumtaja Allah ili kuepukana na fitna.
4- Mada hii inazungumzia: Nyumba ni nyenzo kubwa ya kujenga jamii ya kiislam na kutoa wanachuoni pamoja na wanawake wema, pia imezungumzia umuhimu wa mzazi kuwaombea dua ya kheri wanae.